ASSAs

MH. BITEKO: MBUNGE WA CCM BUKOMBE AWAPA HONGERA NZITO WANANCHI WAKE

303
0
Share:

Enyi watu wema wa Bukombe, nawapenda sana! Mwakilishi wenu najivunia kuwa sehemu yenu ninyi mlio wengi. 


Nimewaona mnavyoshiriki katika ujenzi wa zahanati yetu ya Bulangwa. Nimewaona kwa wingi wenu Bila kujali umri na jinsia zenu. Nazisikia sauti zenu..
..”Tunataka maendeleo, Tunataka Maendeleo, Tunataka Maendeleo”….
Nimesikia imani yenu kuwa maendeleo yetu yapo mikononi mwetu, pamoja tutaendeleza wilaya yetu na nchi yetu.


Hivi ndivyo walivyofanya wazee wetu kwenye mashamba ya ushirika na nguvu kazi ndo tukapata hata shule zile, zahanati zile ofisi zile nk.
Kama mwakilishi wenu mnanipa nguvu mpya, Hamasa mpya na moyo mkuu…..Tutafika!
Kusema na Kutenda daima iwe msingi wetu.

(Visited 19 times, 1 visits today)
Share this post