ASSAs

‘MIMI NI KAMA MFUNGWA MTARAJIWA’ RAIS MAGUFULI

1379
0
Share:

Rais wa Tanzania, John Magufuli ametoa zawadi ya ng’ombe watatu na magunia 15 ya mchele kwa wafungwa na mahabusu katika Gezeza Kuu la Butimba jijini Mwanza akisema na yeye ni kama mfungwa mtarajiwa.


Rais Magufuli ametoa zawadi hiyo leo Jumanne Julai 16, 2019 baada ya kutembelea gereza hilo na kuzungumza na wafungwa, mahabusu na askari wa Jeshi la Magereza waliomueleza kero mbalimbali zinazowakabili.


“Mimi kama mfungwa mtarajiwa hapa ni mtakuja nasema uongo? Wanakula magunia mangapi kwa siku gunia 13,” amehoji Magufuli akitaka kujua kiwango cha chakula wanachokula wafungwa hao kwa siku, baada ya kutajiwa idadi hiyo ya magunia alionyesha kushangazwa.


“Nitaleta magunia 15 na ng’ombe watatu. Nawaomba mkuu wa magereza hawa ni vijana wenu, siku hiyo chinjeni ng’ombe na mpike mchele mle, nyinyi askari pamoja na hawa vijana katika kula pamoja ndio tunaujenga upendo wa Mungu na upendo wa kweli” amesema Magufuli.

(Visited 303 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us