ASSAs

IDARA YA ARDHI TEMEKE, YALALAMIKIWA KWA RUSHWA

862
0
Share:

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke imesema kuwa katika kipindi cha mwezi April hadi Juni 2019 imeokoa kiasi cha shilingi millioni 10, 440,748 kutoka katika majalada ya uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Temeke, Donasian Kessy amesema katika kipindi hicho TAKUKURU ilipokea Taarifa zinazohusika na vitendo vya rushwa 101 huku taasisi zilizoongoza kulalamikiwa ni Manispaa ya Temeke idala ya ardhi .

“Idara ya ardhi imekua ikiongoza kulalamikiwa kuhusu rushwa kwa muhula wa pili,hivuo tumejipanga kufanya uchunguzi wa kuangalia kitu gani hasa ambacho kinasababisha kuongezeka kwa rushwa”amesema Kessy

Amesema kuwa, idara nyengine inayolalamikiwa kwa vitrmdo vya rushwa ni idara ya Afya ,Mazingira, Mahakama katika mabaraza ya ardhi ya wilaya ya Temeke pamoja na polisi.

Hata hivyo,alisema katika majalada mapya ya uchunguzi yaliofunguliwa na kufikia hatua uchunguzi wa kina ni 59 na majalada 7 yakipelekwa katika makao makuu.

” Takukuru Mkoa wa Temeke imefanikiwa kufungua kesi mpya 2 ambapo kesi ya Kwanza ilifunguliwa mahakama ya wilaya Temeke Juni 18 kesi namba CC/02/2019 ambayo inamhusu Castory Kyula ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke idala ya usafi na Mazingira “amesema Kessy

Amesema kuwa, Takukuru Mkoa wa Temeke inaendelea na jukumu la kuelimisha kupitia njia mbalimbali lengo likiwa ni kuwahamasisha Wananchi kushiriki kwa vitendo katika mapambano dhidi ya rushwa.

Aliongeza kuwa,katika kuandaa taifa la vijana wanaoichukia rushwa vikabu 58 vya kupinga rushwa vilifunguliwa na 74 vya zamani vilitembelewa kwa lengo la kuviimarisha.

Katika hatua nyengine amesema wamejipanga vizuri katika kudhibiti rushwa ya ngono katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka

(Visited 68 times, 1 visits today)
Share this post