ASSAs

MAGUFULI AMPONGEZA SPIKA NDUGAI MKOANI DODOMA

772
0
Share:

Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kutokana na kazi aliyoifanya Mbunge wa Kongwa, Spika Job Ndugai atashangaa kuona watu kama hawatampigia makofi.

Rais Magufuli amesema kuwa hatuchagui malaika na mtu akitaka kuchagua malaika afe aende mbinguni atawakuta Malaika huko.

“Kutokana na kazi nzuri anayofanya spika huyu nitashangaa sana kama hamtamshangilia makofi mengi hatuchagui malaika na akitaka mtu kuchagua malaika kufa nenda mbinguni utawakuta malaika huko lakini kwa binadamu nawaaambia kwa maendeleo yenu huyu amesaidia Taifa, ” amesema Rais Magufuli leo akiwa Kongwa jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa “Nafahamu wakati wa kampeni wapo wengine waliotaka ubunge na nilipofika hapa nikawaambia kazi sio ubunge na kweli wale waliogombea na Mh. Ndugai niliwateua nafasi mbalimbali.”

(Visited 63 times, 1 visits today)
Share this post