ASSAs

UTAFITI: WAZAZI CHANZO CHA UKATILI

656
0
Share:

Imebainika kuwa endapo wazazi hawatokua karibu kuzungumza na watoto wao itapelekea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kuongezeka kutokana na watoto hao kukosa fursa ya kuelezea changamoto zao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii Mkurugenzi wa taasisi ya Thrive for Community Elevation Foundation (TCE ) Merry Mangu katika uzinduzi wa kampeni ya ‘malezi chanya’ amesema kuwa wazazi wamekua hawana ukaribu na watoto wao hali ambayo inachangia kuongezeka kwa vitendo vya ukatili.

“Leo tumezi dua kampeni ya ‘malezi chanya’ kwa lengo la kuanzisha jitihada na mkakati endelevu ili kuwafahamisha wazazi, walezi, jamii na Serikali kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kwani umekua ukiongezeka kwa kasi ” amesema Merry

Amesema kuwa, kutokana na hali ya ongezeko la ukatili wa watoto wamejipanga kuifikia mikoa saba ambayo imeathirika zaidi na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto ikiwa ni Dar es Salaam,Mbeya,Mwanza,Simiyu, Arusha,Kilimanjaro, Tabora na Singida.

Ameongeza kuwa, kulingana na ripoti ya mwaka 2017/18 ya Jeshi la Polisi na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) imeripotiwa matukio ya ukiukwaji wa haki za watoto iliongezeka kutoka matukio 4728 katikati ya mwaka 2017 mpaka kufikia matukio 6376 katikati 2018 .

“Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto hasa katika mfumo wa ubakaji na kulawiti ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadam ulioongoza kwa mwaka 2018 ambapo tatizo hilo limetajwa kutokea katika wilaya 20 katika mikoa 10 ya Tanzania ” amesema Merry

Hata hivyo, amesema kuwa, wahanga wengi katika matukio ya ukatili dhidi ya watoto ni kati ya miaka 7 hadi 14 ambapo vitendo hivyo hufanywa na ndugu wa karibu ambapo matukio hayo hayaripotiwi popote na hatimae husuluhishwa na familia.

Kwa upande wake, Mwasisi wa TAMASHA shirika la Vijana, Richard S Mabala amesema kuwa, matatizo mengi yanatokea katika familia kutokana na wazazi kukosa fursa ya kukaa karibu na watoto wao ili kuweza kuzungumza nao kujua changamoto zao zinazowakabili.

“Mimi nataka tuanzishe kampeni maalum kwa ajili ya wa baba kwani imeonekana watoto wakiume wanakosa kukaa na Baba karibu hali inayopelekea kujiingiza kwenye vitendo ambavyo havifai ikilinganishwa na mwanamke yeye anapata fursa ya kukaa na mama jikoni “amesema Mabala.

Naye, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Rahim Ndambo amesema kuwa, lengo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kuweka jitihada za kuijenga jamii bora na yenye ustawi chanya ili kuchochea Maendeleo endelevu katika maeneo manne ikiwa ni elimu ,Afya, Mazingira na uwezeshaji kiuchumi.

(Visited 43 times, 1 visits today)
Share this post