ASSAs

‘WATENDAJI WA ARDHI SIWATISHI’ LUKUVI

422
0
Share:

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi leo July 18, 2019 amezungumza na Wataalam wa Ardhi ikiwa ni katika uboreshaji wa Wizara hiyo katika utendaji kwa Wananchi.

Lukuvi amesema “Ndugu zangu watendaji wa ardhi siwatishi, sina uhakika kama mwakani nikienda kugombea na kurudi kama nitakuja Wizara hii, lazima niwaambie ukweli hapa sasa mmeingia katika kumi na nane zangu, mimi ni eyes on hands on”

“Nipo na nyinyi nitakula sahani moja na nyinyi mimi sivumilii mtu, katika kipindi changu katika Wizara hii nimeona madudu makubwa mnayofanya, mnafanya mambo ya hovyo sana, inawezekanaje watu wazima mnamilikisha kiwanja kimoja kwa watu watatu na mmesoma, ndugu zanguni mambo haya mnayafanya sana acheni mtaungua” Lukuvi

(Visited 25 times, 1 visits today)
Share this post