ASSAs

WAZIRI BASHUNGWA AAHIDI KUTATUA KERO ZA WAFANYABIASHARA

531
0
Share:

Waziri Wa Viwanda na Biashara Inocent Bashungwa amesema serikali imeweka mikakati endelevu katika kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara Wa soko la kariakoo ili kusaidia Kuinua Uchumi Wa Nchi

Kauli hiyo ameitoa mapema leo Jijini Dar es salaam katika Mkutano uliojumuisha wafanyabiashara wa kariakoo ambapo amesema ataweka jitihada za kusikiliza kero zote na kuangalia kwa makini vikwazo pamoja na kuangalia sheria pamoja na vikwazo ambavyo hupelekea wafanyabiashara hao kulalamika kila siku

Amesema kuwa, wafanyabiashara wengi wamekuwa wakilalamikia hususani bàadhi ya kodi ambazo wamekuwa wakitozwa mizigo yao hata kabla hawajauza na kupata faida na kusababisha baadhi yao kuacha majengo na kukimbia kodi hizo hivyo kupelekea Taifa kukosa mapato

Kwa Upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Wakala Wa Usajili Wa Makampuni BRELLAna Emanuel kakwezi amesema kupitia mkutano huo itasaidia wao kuwa karibu na Wamachinga na kuwarasimisha badala kila kukicha kushinda barabarani badala take kuwasadia nao wakue kibiashara .

Aidha amesema watajitahidi wanashughulikia kero iliyolalamikiwa na baadhi ya wazalishaji Wa bidhaa kuhusu kukopiwa bidhaa zao na baadhi ya wafanyabiashara ambao sio waadilifu hivyo kupelekea kukosa wateja.

Nao Baadhi ya wafanyabiashara hao akiwemo Mary Mgaya ,Zacharias Andrew wamemshukuru Waziri kwa kuwaita kwa pamoja na kuwasikiliza changamoto zao hivyo wanategemea kupitia yeye baadhi ya kero zao zitatatuliwa

Aidha wito umetolew kwa baadhi ya Wafanyabiashara kuhudhuria kesho katika ofisi ndogo ya Wizara ya Viwanda na Biashara iwakakutane na Mamlaka kukusanya kodi TRA,Wakala Wa Forodha TAFFA, ili wakatoe malalamiko yao na kutatuliwa kwa wakati na Mazingira yao yaweze kuimarishwa.

(Visited 48 times, 1 visits today)
Share this post