ASSAs

LUSINDE AMPA 5 MUSIBA,AWAJIA JUU KINANA NA MAKAMBA, AMTAKA LUGOLA KUMUHOJI NAPE

784
0
Share:

Dar es Salaam

Mbunge wa jimbo la Mtera na mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa CCM,Livingston Lusinde amewataka viongozi wastaafu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na Yussuf Makamba kuacha tabia ya kulalamika kuhusu kutukanwa na mwanaharakati huru Cyprian Musiba na kuifanya kuwa ishu ya Taifa bali wadili nae mwenyewe.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku chache baada ya viongozi hao wastaafu kuandika waraka wa malalamiko kwa baraza la wazee kuhusiana na kutukanwa na mwanaharakati huyo.

Amesema kuwa, kitendo anacho kifanya Cyprian Musiba anakiunga mkono kutokana na mazingira ya kutukana viongozi waliyatengezana wao wenyewe wakiwa viongozi ndani ya chama cha Mapunduzi CCM.

“Nawashangaa sana Kinana na Makamba wanavyolalamika kwani hili dude wameliunga wao wenyewe kwani Nape alipata umaruufu kwa nini? Si alikua akiwatukana na kuwakashifu viongozi wenzake akiwemo Waziri mkuu mstaaafui Edowardo Lowasa, au leo wamesahau “alihoji Lusinde.

Aidha amesema, anachukizwa na kitendo cha Mbunge wa Mtama Nape Nauye kumwita Rais John Maguful mshamba, kwani amefanya mambo mengi ya maendeleo ya wananchi ikiwemo ujenzi wa daraja la salenda, ndege,kuboresha miundombinu ya barabara, maji na Nishati pamoja utanuzi wa kiwanja cha ndege kimataifa cha Mwalimu Nyerere.

” Hivi kweli mshamba anaweza kuleta mageuzi makubwa kiasi hichi ? amewatumbua viongozi wazembe ambao walikua wakila mali za umma baada ya mianya rushwa kufungwa ndio wanaanza kulalamika ” alihoji Lusinde.

Aidha amemuomba Rais John Magufuli kuruhusu waraka uliofanyiwa uchunguzi na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally kusomwa na kurushwa kwenye vyombo vya habari ili wananchi waweze kuona uwozo uliokua ukifanywa na hao viongozi wanaojiita waadilifu.

Hata hivyo, amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Kangi Lugola kuwahoji viongozi wote wanaomdhalilisha na kumtukana Rais John Magufuli ili waweze kuelezea dhamira yao ya kutoa matusi hayo ni nini.

Amesema kuwa, kelele nyingi zinazopigwa sasa hivi ni kutokana na uchaguzi wa Serikali za mitaa kukaribia wanataka kuukwamisha lakini kwa mambo aliyoyafanya Rais Dkt John Magufuli haina shaka ushindi lazima.

Amesema kuwa, licha ya Kazi kubwa iliyokua inafanywa na aliyekua Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu Itikadi siasa uenezi Nape Nnauye lakini haishi viongozi waliopo sasa wanafanya kazi kubwa zaidi ya waliopita.

(Visited 98 times, 1 visits today)
Share this post