ASSAs

BAKWATA YAWATAKA MAHUJAJI KUTOJIHUSISHA NA VITENDO VISIVOFAA

790
0
Share:

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka mahujaji nchini kutumia safari za hijja kutekeleza ibada na kutojihusisha na vitendo visivyofaa ikiwamo kuzungumzia mambo ya kisiasa pamoja na kusema uongo

Hayo yamebainishwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Bin Zuber wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya mahujaji yaliyoandaliwa na Idara ya Hijja Makao Makuu wanaotarajiwa kuanza safari kwenda Makka na Madina, Agosti 4, mwaka huu.

Sheikh Zuberi amesema, kila hujaji kabla ya safari ni lazima atie nia kitu gani anakifuata katika ibada hiyo ili kujenga mahusiano makubwa na Mwenyezi Mungu, ambapo kinyume na matakwa hayo Mungu hawezi kupokea ibada zao endapo wataenda kujishughulisha na kujiingiza kwenye mambo machafu.

“Nawambieni maana ya hijaa ni kuomba rehema ya msamaha matendo tuliyoyafanya haitapendeza endapo mtafika huko na kuanza kuzungumzia siasa hili halitampendeza Mwenyezi Mungu,cha msingi ni kuhakikisha munakuwa watulivu na kuacha maovu muliyokuwa mukiyafanya hapa nchini ambayo mengi yanawatenga na Mungu.”amesema Zuberi.

Ameongeza “Kikubwa mukiwa huko nawaombeni mjikitize zaidi katika ibada kwani hiyo ndiyo nguzo ya tano ya uislam pamoja na kuombea nchi amani na Rais Dk.John Magufuli ili hata mkirejea muwe na amani pia,”

Hata hivyo, amesema kwenda hijja na kutafuta zawadi, biashara za kihalali si mbaya kwani hata maandiko matakatifu yameruhusu kujishughulisha na ujasiriamali.

Amesema kwa mwaka huu Tanzania Baraza na Visiwani wamejipanga kuondoa changamoto zinazojitokeza katika miaka iliyopita ambapo Hadi Sasa Kamati ya maandalizi imeshasafiri kwenda Makka kwa lengo la kuwapokea mahujaji watakaoanza safari kuanzia Agosti 4, mwaka huu.

“Taasisi zote zinazowakabili mahujaji mwaka huu zimepitishwa rasmi na watashirikiana na balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia ili kuhakikisha majujaji wanafika na kufanya ibada yao kwa amani ikiwa ni pamoja na kurejea nchini salama,”amesema Sheikh Zuberi.

Amesema hadi sasa tayari wamesajili mahujaji 110 ambapo wanataraji kusajili mahujaji 2,000, wengi wao wapo mikoani lengo lao ni kusafirisha mahujaji 120 na usajili bado unaendelea, huku akiwataka mahujaji kuzingatia maelekezo wanayopewa na viongozi wao ili kuondokana na usumbufu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Hija
Bakwata Alhaj Haidari Kambwili amesema mahujaji hao watarejea nchini Agosti 25, na wamejipanga kuhakikisha hawapati usumbufu wa makazi.

Naye, Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shehe Hamid Jongo aliwasisitiza hijja hiyo itumike kiibada zaidi na kuweka kando mazungumzo ya kisiasa.

Ameongeza kuwa, gharama za hijja kwa mwaka huu ni kwa wanaoanza ni dola 4300 na watakaorudia ni dola 4500, ambapo Mungu anatambua mambo yaliyo ya kheri huku aliwataka wajikite zaidi kuomba msamaha, afya njema na amani.

(Visited 60 times, 1 visits today)
Share this post