ASSAs

DC ILALA AZINDUA KAMATI YA HAMASA MAPOKEZI YA SADC

617
0
Share:


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amezindua Kamati ya Hamasa kwa ajili ya mapokezi ya viongozi wa SADC ambao wanatarajia kufanya mkutano mwezi Agosti Mwaka huu Wilayani Ilala.

Katika uzinduzi huo ambao ulifanyika Dar es Salaam leo Mjema alisema katika Kamati hiyo imewashirikisha Waandishi wa habari ,warembo lengo kutoa hamasa katika kuelekea katika mkutano mkuu wa Maendeleo ya Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC.

“Leo (jana)nimezindua kamati maalum kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa SADC nitakuwa na timu Maalum ya kusimamia viongozi wa marais wakitoa burudani mbalimbali”alisema Mjema.

Alitaja baadhi ya wanakamati katika upande wa hamasa atakuwepo Zamaradi Mtetema,Basila Mwanukuzi,Hoyce Temu watawaongoza Wake wa marais katika onyesho maalum .

Pia alisema wasanii mbalimbali watakuwepo kutoa burudani kila njia panda kuanzia Uwanja Ndege,Vingunguti,Tazara hadi Serena hoteli.

“Tukio hili la Wageni wa mkutano mkuu SADC mimi ndio mwenyeji katika Wlaya yangu ya Ilala hivyo lazima shamra shamra ziwepo tukio ni la nchi nzima mwaka huu Mwenyeji wa Mkutano huo Rais John Magufuli ndio Mwenyekiti.

Alisema kuanzia Agosti 5 wataanza kupokea wageni mbalimbali ambao wanakuja kwa ajili ya Mkutano huo ni faraja kubwa kwa nchi yetu katika kupokea ugeni huu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Jumanne Shauri amewataka wafanyabiashara wa nyumba za Wageni kupaka rangi majengo yao yawe masafi na majengo ya barabarani yote yapakwe rangi.

Mkurugenzi shauri aliwataka wafanyabiashara waendelee na shughuli zao kama kawaida na wale waliopata fursa kufanya biashara watumie vyema katika kuitangaza Ilala .

(Visited 62 times, 1 visits today)
Share this post