ASSAs

MANISPAA YA ILALA YADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI

686
0
Share:

NA HERI SHABAN

MANISPAA Ilala imezindua wiki ya unyonyeshaji maziwa ya Mama kwa Mtoto.

Madhimisho hayo kuwa yanafanyika kila mwaka mwezi Agosti na Tanzania huungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama.

Akizungumza katika viwanja vyake Arnatoglou Manispaa ya Ilala leo Ofisa Lishe wa Halmashauri ya Ilala Frola Mgimba alisema malengo ya wiki ya unyonyeshaji Duniani mwaka 2019 ni kuinua uelewa kuhusiana na jamii jinsi ya usawa wa kijinsia, sheria na kanuni zinazowezesha kulinda, kuendeleza na kusaidia unyonyeshaji wa maziwa ya mama na hivyo kuboresha usawa wa kijinsia katika ngazi zote ili kusaidia kulinda na kuendeleza unyonyeshaji.

Aidha Frola alisema malengo mengine ya siku hii ni kuhimiza uimalishaji wa usawa wa kijinsia, usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni zinazosaidia kulinda, kuendeleza na kusaidia unyonyeshaji wa maziwa ya mama na hivyo kuboresha lishe kwa jamii.

Alisema wiki hii ya unyonyeshaji inaanza Agosti mosi hadi Agosti 7 kila mwaka na kwa mwaka huu 2019 kauli mbiu ya maadhimisho hayo itakuwa “Waweshe Wazazi kufanikisha Unyonyeshaji “.

Akielezea baadhi ya faida ya unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama kwa Watoto ni unyonyeshaji wa maziwa ya mama huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha afya, kulinda uhai wa maisha ya mtoto, kunyonyesha maziwa pekee katika miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto ndio njia bora na salama ya kumpatia mtoto virutubisho vyote muhimu kwa ukuaji na maendeleo yake.

Alitaja faida zingine maziwa ya mama yana sifa ya kipekee ya kuwa na kinga mwili ambazo umkinga mtoto dhidi ya magonjwa mbalimbali hivyo kuchangia katika kupunguza vifo vya watoto wachanga na walio katika umri wa miaka mitano.

Frola alisema kunyonyesha pia kuna faida kubwa kwa mtoto kunajenga mahusiano katika ya mama na mtoto hivyo kumjenga mtoto kijamii zaidi.

Aliwataka wazazi mara baada ya kujifungua Mama na mtoto anashauriwa wagusane ngozi kwa ngozi, wanyonyeshe mtoto ndani ya saa moja baada ya kujifungua .

Pia Mama anashauriwa ndani ya miezi sita usimpe maji au vyakula vingine badala yake mtoto mama unashauriwa kumpa maziwa pekee kwa miezi sita.

(Visited 73 times, 1 visits today)
Share this post