ASSAs

Mbunge ZUNGU AMFAGILIA MKURUGENZI WA ILALA

622
0
Share:

MBUNGE wa Ilala Mussa Zungu amempongeza Mkurugenzi wa Ilala Jumanne Shauri kwa kutatua kero katika soko la Ilala .Zungu alitoa pongezi hizo leo katika ziara ya viongozi wa Halmashauri ya Ilala waliofika sokoni kutatua kero.Akizungumza katika ziara hiyo leo alisema kuwa jana alifanya ziara sokoni hapo na kukuta mazingira mengine sio mazuri akalazimika kuzibeba kero hizo na kuwasilisha kwa mkurugenzi wa Ilala na leo ametatua changamoto.”Tunakupongeza Mkurugenzi wa Ilala Jumanne Shauri kwa msaada wa mabati 200 yatatue kero katika soko hili ,na pongezi zingine zimfikie Rais John Magufuli kwa kutuletea Mkurugenzi jembe pia Msikivu kero anatatua kwa wakati”alisema Zungu.Zungu alisema soko hilo linategemewa na wafanyabiashara wa Ilala na nje ya Ilala likitengenezwa sehemu ya chanzo cha mapato makubwa.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ilala Jumanne Shauri alisema ofisi yake kwa sasa itakabidhi bati 200 na itakuwa inaboresha kila wakati wakati wakisubiri kujenga soko la kisasa.Shauri alisema mpango wa halmashauri kujenga soko la Kisutu mara baada ya kisutu kumalizika watajenga soko la Ilala na Buguruni yote yawe ya kisasa.”Katika halmashauri ya Ilala tuna jumla ya masoko 26 ya jumla na rejareja dhumuni la halmashauri yangu wananchi wote wa Ilala kuwasogezea huduma za jamii katika maeneo yao ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM “.alisema Shauri.

Katika hatua nyingine Shauri aliagiza Mhandisi wa Manispaa ya Ilala kuweka kambi katika soko hilo kwa siku nne ili kufanya ukaguzi wa kina kwa ajili ya kuangalia athari zake.Wakati huohuo Mkurugenzi wa Ilala aliwataka Mama Lishe wa Ilala kuunda vikundi vyao ili waweze kupata mikopo ya serikali.Alisema Jumatatu atakabidhi bati katika soko hilo ataongozana na Maofisa wake akiwemo Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Ilala .Naye Diwani wa Ilala Saddy Kimji alisema soko la Ilala limejengwa mwaka 1945 linategemewa na wakazi wa halmashauri ya Ilala na Dar es Salaam kwa ujumla.Diwani Kimji aliomba lijengwe soko la kisasa na kuboresha miundombinu ya soko hilo nyakati za mvua kero inakuwa kubwa ..mwishoZiara mbunge wa Ilala Mkurugenzi na Diwani wa Ilala soko la Ilala leoAgosti 03/2019

(Visited 54 times, 1 visits today)
Share this post