ASSAs

BOHARI YA DAWA YAKABIDHI VIFAA TIBA MUHIMBILI

410
0
Share:

Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi dawa na vifaa tiba kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kwa ajili ya kuwahudumia majeruhi wa ajali ya moto waliohamishiwa hospitalini hapo kutoka mkoani Morogoro.

Makabidhiano haya ya dawa ni mwitikio wa maombi ya dharura yaliyoombwa na Hospitali Muhimbili kwa ajili na majeruhi hao.

Meneja wa MSD, Kanda ya Dar es Salaam Bw. Celestine Haule amesema mpaka sasa jumla ya shehena ya malori matano yameshakabidhiwa Muhimbili zikiwemo dawa muhimu zinazotumika kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi hao.

(Visited 15 times, 1 visits today)
Share this post