DOGO JANJA AWEKA BAYANA PENZI JIPYA

Msanii wa Hip Hop nchini, Dogo Janja amemuweka wazi mpenzi wake mpya
baada ya muda mrefu kupita tangu alipoachana na aliyekuwa mke wake,
muigizaji Irene Uwoya.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dogo Janja ameweka picha akiwa na
mpenzi wake huyo mpya siku ya jana kwenye sikukuu ya Eid El Hajj na
kuandika, “kipande hiki EID tunaimaliza kwa style hii.. happy moments
with my baby!! Kenya 254 wagwaan”.
Hii sio mara ya kwanza kwa Dogo Janja kumuonyesha mpenzi wake huyo
katika mtandao wa kijamii wa Instagram, huwa anam-post mara kwa mara
huku akiandika maandishi yanayoashiria wana mahusiano.
Huyu anaweza akawa mrithi wa aliyekuwa mke wake, Irene Uwoya ambaye
waliachana mwaka jana baada ya kudumu kwa kipindi kifupi kwenye ndoa.
Pia Dogo Janja aliwahi kusema yupo tayari kuoa tena mwanamke mwingine.