ASSAs

‘HATA KAMA NITASHIKA MKONGOJO NITAIMBA NA WATU WATAINUKA’ KHADIJA KOPA

412
0
Share:

Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa, amesema anaamini ule usemi usemao; “ng’ombe hazeeki maini” ambapo amesema hata akizeeka bado sauti yake itakuwa na ladha ileile.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Khadija alisema kuwa kitu kikubwa anachojivunia ni sauti nzuri aliyopewa na Mwenyezi Mungu ambayo alikuwa nayo tangu akiwa msichana mdogo mpaka leo haijabadilika na haitaweza kubadilika mpaka anashika mkongojo.

“Yaani naelekea uzeeni lakini sauti yangu iko palepale haijawahi kuharibika na kamwe haitatokea hivyo hata kama nitashika mkongojo nitaimba na watu watainuka kwenye viti vyao na hiyo ndio maana ya kuitwa malkia,” alisema Khadija

(Visited 40 times, 1 visits today)
Share this post