ASSAs

DAS ASENGA AZINDUA KAMPENI YA TOKOMEZA TRACHOMA WILAYANI ROMBO

985
0
Share:

TOKOMEZA TRACHOMA WILAYANI ROMBO NDANI YA MWAKA 2019.

Ni ugonjwa wa Macho unaoenezwa na NZI kwa kusambaza wadudu kutoka katika jicho na muathirika Kupeleka Katika Jicho la Mtu Mwingine na kupelekea kope kujikunja na kuharibu jicho.

Mgonjwa asipotibiwa mapema upata upofu,tiba yake Ni kwa kufanya upasuaji mdogo.

Njia Rahisi ya kujikinga na ugonjwa huu Ni usafi wa mazingira hasa kunawa kwa maji safi na usafi wa vyoo na maeneo yote yenye INZI wengi.

Leo Jumamosi Tarehe 17/08/2019.
Akizindua Kampeni Maalumu kwa Wilaya ya Rombo ya kuwatibu wagonjwa 246 waliopatikana baada ya utafiti.
Bwana Abubakar Asenga Ambae Ni Katibu Tawala Wilaya ya Rombo(DAS) akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, aliishukuru Taasisi ya KILIMANJARO CENTER FOR COMMUNITY OPHTHALMOLOGY (KCCO), inayofadhili gharama za Matibabu kwa wagonjwa hao.

Aliwataka Maafisa Taarfa wote walioshiriki semina hiyo kuhakikisha wanatoa Ushirikiano wa kutosha wakila hali ili kuhakikisha TRACHOMA Inatokomezwa Wilayani Rombo.

Aidha kutokana na Tanzania kuanza upandikizaji wa Macho ili kupambana na Upofu,Bwana Asenga liiomba jamii kuanza kuelimika na kubadilika kwa kukubali pale ndugu yao anapofariki baadhi ya viungo viweze kutumika kuwasaidia waliokuwa hai,

Alisema
“Daktari amesema hapa wanaorodha ya watu 800 wa kubadilishiwa mboni za Macho,hakuna kiwanda cha kutengeneza Macho Bali Ni kama kuchangia damu ama Figo,

Inapotokea mtu mzima mwenye afya amefariki mfano kwa ajali lazima tujiulize kipi Ni faida kumzika na macho,Moyo,figo na ini lake ama vitu hivyo vichukuliwe kumsaidia baba yake aliebaki hai? apone upofu ama abadilishiwe figo?HILI NI SWALI LA KITAIFA LAZIMA TUJADILIANE,Kwanini Watanzania wanakimbilia India kufata vitu hivyo,

Ni kwa sababu wenzetu India wanasheria za kuchukua baadhi ya vioungo kwa Maiti ili kusaidia wengine,kama kweli tunataka kupunguza Gharama za Matibabu na hasa watu kusafiri kwenda nje lazima sasa tuweke utaratibu na Mimi nipo tayari kusaini ikitokea Nimekufa basi kiungo changu kinachofaa kitolewe kusaidia wengine kuliko kiende kuoza chini ya ardhi.

Nawashukuru sana KAMPENI IMEZENDULIWA RASMI”
Mwisho wa Kunukuu..

(Visited 95 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us