ASSAs

MUUNGANO WA UPINZANI NA BARAZA LA MAJESHI WASAINI MAKUBALIANO YA SERIKALI YA MPITO

448
0
Share:

Leo jumamosi August 17, 2019 huko Nchini Sudan ya kaskazini, Muungano mkuu wa upinzani na Baraza kuu la Jeshi wamesaini makubaliano ya  serikali ya mpito.

Zoezi hilo la mpango wa kuwa na utawala wa kiraia utakaotawala kwa miezi 39 ya kipindi cha mpito limefanyika katika ukumbi wa Naeli katika mji mkuu Khartoum mbele ya wakuu wa Kitaifa na kimataifa akiwemo waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed na Rais wa Sudan ya kusini Mh. Salva Kiir.

Katika makubaliano hayo, Baraza la pamoja la wanajeshi na raia 11ambalo lnatarajiwa kutawala kwa zaidi ya miaka mitatu (miezi 39) hadi hapo kila kitu kitakapo kuwa sawa na kufuatiwa na uchaguzi mkuu utakaofanyika kwa njia ya kidemokrasia.

Pia kutaanzishwa chombo cha kutunga sheria na Baraza la Mawaziri litakaloteuliwa na wanaharakati na kutawaliwa na raia na muundo wa Baraza kuu la mpito la kiraia linatarajiwa kutangazwa hapo kesho Jumapili.

Huenda ni bidii za Rais wa Sudan kusini Salva Kiir ndo zimefanikiwa maana kwa zaidi ya siku tatu tangu tarehe 14 August alilipotiwa kuwasili Sudan kaskazini ili kukutana na baadhi ya viongozi wa mapigano Darfur JEM Dr Gibril Ibrahim Mohammed kwa ajili ya juhudi za kurudisha amani nchini humo.

Africanews.com

(Visited 37 times, 1 visits today)
Share this post