ASSAs

NCHI 16 ZA SADC ZIMEKUBALI NA KUPITISHA KISWAHILI KUWA LUGHA RASMI.

959
0
Share:

Kufuatia vikao vinavyoendelea vya Umoja wa Maendeleo ya  nchi za ukanda wa kusini mwa Africa (SADC) nchini Tanzania Jijin Dar es salaam katika ukumbi wa Mwl Julius Nyerere, leo Jumamosi August 17, 2019 wameadhimia na kuipitisha kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ya Umoja huo baada ya Kiingereza,Kireno na Kifaransa.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje nchini Tanzania Prof. Paramagamba Kabudi amesema kufuatia utafiti wa wa kituo cha utafiti wa nyaraka cha kusini mwa Afrika, Kiswahili kimepitishwa kwanza kama lugha rasmi ya mawasiliano ya  mdomo kabla ya kupitishwa tena kwa  ajili ya mawasiliano ya maandishi.

Kama mwenyekiti wa mkutano huo wa 39 wa viongozi wa nchi 16 za umoja wa SADC, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Joseph Magufuli wakati wa ufunguzi alinukuliwa akisema “Ni wito wenye sifa nzuri ya kufuatilia kwa haraka na kupitishwa kwa  Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha nne rasmi za umoja wa SADC”

Kiswahili ni lugha rasmi ya kitaifa inayozungumzwa nchini Tanzania na ukanda wote wa Afrika mashariki tangu enzi hizo ila kutokana na mabadiliko na ukuaji wa maendeleo ya kitekinolojia, utawala shughuli za kisiasa, shughuli za kibiashara, mikutano ya kitaifa na kimataifa, masuala ya Elimu, shughuli za kiutamaduni, muziki na sherehe  na lugha za vyombo vya habari hadi kufikia karne ya 20-21 lugha ya Kiswahili imendelea kukua kiasi cha kuvuka mipaka na kuanza kutumiwa na nchi za afrika ya kati.

(Visited 279 times, 1 visits today)
Share this post