ASSAs

Naibu Waziri Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Balozi Wa Umoja Wa Ulaya, Nchini Botswana

825
0
Share:

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Botswana, Jan SADEK walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo baina yao yalijikita kwenye masuala mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Sambamba na hayo katika mazungumzo hayo Dkt. Ndumbaro aliendelea kumueleza Balozi Jan, juu ya umuhimu wa Umoja wa Ulaya kutekeleka wito alioutoa Rais Magufuli wakati wa Mkutano wa SADC kuhusu kuiondolea nchi ya Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi. Balozi Jan alikuwa nchini kuhudhuria Mkutano wa SADC.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza alipokutana kwa mazungumzo na Balozi Jan. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akisisitiza jambo alipokutana kwa mazungumzo na Balozi Jan.

(Visited 87 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us