ASSAs

MZUNGU ALIYESABABISHA NDEGE YA ATCL KUZUILIWA A.KUSINI HUYU HAPA

3097
0
Share:

Huyu ndiye yule mzungu maarufu wilayani Monduli aliyekuwa anatumia ugoro wa Kimaasai kunusa na kuubwia mdomoni kila anapokuwa na Wamaasai. …

Kitendo hicho kikampatia jina maarufu la Bwana Ugoro ambaye alikuwa anamiliki Hekta laki nne wilayani Monduli kuanzia Makuyuni hadi Loolkisale. …

Alikuwa na trekta mia tatu. …harvesters kadhaa. …Landrovers zaidi ya 50. ….

Helikopta kadhaa za kupeleka wafanyakazi na maafisa kilimo mashambani na kupigia dawa mazao pamoja na kufukuzia kwelea kwelea waharibifu wa mazao. …

Alikuwa na ng’ombe wa maziwa wa kisasa zaidi ya elfu mbili na ushee. …

Mwl Nyerere alipotaifisha hilo shamba lake na kuwagawia Wamaasai Bwana Ugoro au kwa jina lake halisi Hermannus Phillipus Steyn Kaburu mwenye asili ya Uholanzi aliikamata Meli yetu ya Kampuni ya NASACO ambayo ilikuwa safarini Ulaya kama mara hii mtoto wake alivyofanya kwa ndege yetu aina ya Airbus. ….

(Visited 1,083 times, 1 visits today)
Share this post