ASSAs

SERIKALI YAANZA MKAKATI WA KUFUTA KESI ZA WANUNUZI WA TUMBAKU

620
0
Share:

Dodoma,

Naibu Waziri wa Kilimo, Husein Bashe amesema moja ya vikwazo vilivyokuwa vinasababisha Sekta ya Kilimo kushindwa kuendelea ni pamoja na Migogoro na kesi za muda mrefu dhidi ya Makampuni za Kilimo ambapo Serikali imedhamiria kufuta kesi zote ili Kampuni hizo ziweze kununua Mazao

Bashe amesema kampuni zilikuwa zikidaiwa zaidi ya Tsh. Trilioni 10 na serikali hali ambayo ilikuwa inasababisha kushindwa kwenda kutoa huduma kwa wakulima

Aidha, amesema wamekubaliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa ndani ya siku 90 Kuanzia leo Septemba 4 suala la madai kwa Kampuni 4 za Kilimo litakuwa limeisha ili kampuni hizo ziendelee kununua mazao kwa wakulima.

Pia, amesema kuna zaidi ya kilo Milioni 12 za Tumbaku zipo mikononi mwa Wakulima na kampuni za kilimo chini ya Bodi ya Tumbaku Tanzania zitakutana na wakulima kununua kilo hizo kuanzia Septemba 12.

(Visited 64 times, 1 visits today)
Share this post