ASSAs

HARMORAPA AMJIBU LULU DIVA SUALA LA UMRI

1059
0
Share:

Wiki iliyopita ilitrend habari inayomhusu msanii Lulu Diva baada ya kuhojiwa na kuhojiwa na kituo cha EATV na kusema kwa sasa ana umri wa miaka 19 na atarajiwa kuolewa akifikisha miaka 25.

Leo limeibuka lingine katika kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa msanii Harmorapa ambaye ameandika kuwa amefikisha umri wa miaka 9 ikiwa ni miaka 10 pungufu ya Lulu Diva.

Harmorapa ameweka wazi kwamba ana umri huo baada ya kupost picha katika mtandao wa kijamii kisha kuandika,

“Namshukuru Mungu siku kama ya leo mwaka 2011 nilizaliwa kijana wenu Athumani Omary a.k.a supa staa Harmorapa, nawaomba muungane kunitakia kheri ya kusheherekea kwa kutimiza miaka 9 ya kuzaliwa”.

Tulijaribu kumtafuta Harmorapa ili alitolee ufafanuzi kwa nini aliandika ana miaka 9 hali ya kuwa anaonekana mkubwa kuliko umri huo lakini hatukuweza kumpata.

Aidha rapa Nikki Wa Pili aliwahi kusema sababu za mastaa kudanganya umri zinatokana na kibiashara zaidi au mtu anaweza akakujaji kutokana na umri wako.

 

(Visited 88 times, 1 visits today)
Share this post