ASSAs

KUMBILAMOTO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SOKO LA PUGU

514
0
Share:

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala mh Omary KumbiLamoto amefanya ziara katika Mnada wa mifugo Pugu na kufanya usafi na kuhamasisha wafanyabiashara wa maeneo hayo kuitumia fursa ya mikopo ya Halmashauri 10% zisizo na riba.

Kumbilamoto amesema wafanyabiashara wa Pugu wanatakiwa kuchangamkia mikopo ya manispaa kwani haina usumbufu wa riba kama ilivyo mikopo mingine.

“Asilimia 10 ya Manispaa ilipitishwa Bungeni tangu mwaka 2009 lakini ilikua inaishia kwenye Benki Tumbo ya watu wachache, lakini Rais Magufuli amekuja na akaipa kipaumbele kwamba ni lazima watanzania wanufaike nayo” amesema Kumbilamoto.

Aidha Mstahiki Meya amefurahishwa na hali ya usafi wa mazingira katika maeneo ya mnada huo wa Pugu tofauti na alivyotegemea na kuahidi kutatua baadhi ya changamoto za miundombinu zilizopo ndani ya uwezo wake mnadani hapo.

“Nimefika leo hapa kufanya usafi nimefurahishwa sana na hali ya usafi hapa machinjioni nilitegemea ningekuta vinyesi pembezoni mwa Kuta lakini haikua hivyo” amesema

Ikumbukwe barabara za mitaa zimehamishiwa Tarura hivyo mstahiki Meya amesema atafika kuongea na wahusika ili kutengenezwa kwa barabara ya kuingia mnadani hapo.

“Barabara zimehamishwa kwetu zimeamishiwa Tarura hivyo sina uwezo wa kutoa maelekezo ya utengenezaji wa barabara hii ya Pugu, serikali ya sasa sio serikali ya wanasiasa ni serikali ya watendaji hatupigi siasa za porojo porojo, nitaongea na wahusika pia nitafika kwa mkuu wa mkoa Mh Makonda nitahakikisha mpaka jumatano nakuja na jibu kamili kuhusi barabara hii ya Pugu” amesema Mstahiki Meya.

(Visited 48 times, 1 visits today)
Share this post