ASSAs

MWANAFUNZI AJIUA BAADA YA MWALIMU KUMKEJELI DARASANI

783
0
Share:

Jeshi la Polisi nchini Kenya linaendesha uchunguzi juu ya tukio lililopelekea mwanafunzi wa umri wa miaka 14 kujiua saa kadhaa baada ya nguo zake kuloa damu ya hedhi alipokuwa shule, Ijumaa Septemba 6, 2019.

Mama wa Jackline Chepngeno, Beatrice Chepkurui Koech amesema kuwa mtoto wake alikejeliwa na mwalimu wa kike katika Shule ya Msingi Kabiangek baada ya damu hiyo kuchafua nguo zake akiwa darasani.

 “Hakuwa na chochote cha kutumia kuzuia damu hiyo. Wakati damu ilipoloanisha nguo yake, aliamriwa kutoka darasani, asimame nje,” amesema mama huyo.

Kundi la wazazi waliandamana nje ya shule hiyo na kufunga barabara inayoelekea shuleni humo wakishinikiza mwalimu huyo achukuliwe hatua, kabla ya kutawanywa na vyombo vya ulinzi vilivyotumia mabomu ya kutoa machozi.

Baada ya tukio hilo Jackline Chepngeno alirudi nyumbani majira ya saa 4 na 30 asubuhi, ambapo baada ya kuzungumza na mama yake, mzazi huyo alimwambia akachote maji mtoni, ajisafishe, kisha waende wote shule.

Hata hivyo mtoto huyo alitumia mwanya huo alipokwenda mtoni na kujinyonga hadi kufariki dunia.

Mwaka 2017 serikali ya Kenya ilipitisha sheria iliyolenga kutoa taulo za kike bure kwa wanafunzi wote wa shule za msingi wenye uhitaji.

Kwa sasa, kamati ya Bunge ya Kenya inafanya uchunguzi kubaini kwanini mpango huo wa bure ambao unaigharimu serikali takribani TZS 10.4 bilioni kwa mwaka hautekelezwi katika shule zote.

(Visited 77 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us