ASSAs

MSIMU WA 10 WA BBS WAZINDULIWA KWA KISHINDO

1678
0
Share:

Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imetangaza ujio wa msimu wa 10 wa Bongo Star Search (BSS) kupitia chaneli ya StarTimes Swahili. Huu unakuwa ni msimu wa pili mfululizo kwa shindano hilo kuruka kupitia chaneli hiyo.


Bongo Star Search ndilo shindano la kwanza la vipaji nchini Tanzania na mwaka linafikisha jumla ya misimu kumi ya kuvumbua na kukuza vipaji.

Tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2007 BSS imetoa nafasi kwa vijana zaidi ya 200 kuonekana na wengine wamekuwa wasanii nyota katika tasnia ya muziki nchini mfano Kala Jerimiah, Peter Msechu, Walter Chilambo, Frida Amani na wengine wengi.


“Sisi tunawaamini sana watanzania kama wao walivyotuamini na kuchagua kutumia huduma na bidhaa zetu, na kwa kuzingatia hilo tunaendelea kubeba uhalisia wa jamii ya kitanzania na aina ya burudani ambayo wamekuwa wakiifurahia kwa miaka kumi sasa, nazungumzia BSS na vimbwanga vyake. Bw. David Malisa, Meneja Masoko StarTimes Tanzania.


“StarTimes tunajali uchumi wa kila mtanzania na nadhani ni dhahiri kupitia bei zetu hivyo nitangaze rasmi kwamba Bongo Star Search 2019 itapatikana kuanzia kifurushi cha NYOTA ambacho gharama yake ni Tsh 8000 tu kwa watumiaji wa kisimbuzi cha Antenna na Tsh 11,000 tu kwa watumiaji wa kisimbuzi cha Dish.”Aliongeza.


Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark Productions na Jaji Mkuu (Chief Judge) wa BSS, Rita Poulsen alizungumzia ujio wa msimu wa kumi huku akitaja ongezeko la mikoa ambayo itafikiwa na usaili wa shindano hilo.


“Nina furaha sana kwa sababu ni ‘anniversary’ ya miaka 10 ya Bongo Star Search, najivunia vipaji ambavyo tumevileta mbele ya watanzania na kuwapa nafasi vijana hao wa kitanzania kuendeleza maisha ya kimuziki na wengine kufanikiwa nje ya muziki pia”. Rita Poulsen, Jaji Mkuu BSS na Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark Productions.

“Habari njema sana kwa watanzania ni kwamba tumeongeza idadi ya mikoa ambayo itafikiwa na usaili wa BSS mwaka huu, Mwaka huu tunakwenda Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam. Jumla mikoa mitano tofauti na mwaka jana tulipokwenda kwenye mikoa mine pekee”. Alisema Madam Rita.


Usaili wa kwanza utafanyika jijini Arusha tarehe 28 – 29 mwezi huu, Mwanza tarehe 4- 5 Oktoba, Mbeya tarehe 10 – 11 Oktoba, Dodoma tarehe 17 – 18 Oktoba na Dar es Salaam tarehe 23, 24, 25 Oktoba.


Mwaka huu pia kuna mabadiliko katika vipindi vitakavyorushwa kupitia chaneli ya ST Swahili kama ambavyo meneja maudhui wa StarTimes Tanzania Bi Zamaradi Nzowa alivyoeleza.


“Vipindi vyetu vitagawanyika katika makundi mawili ambayo ni ‘highlight’ pamoja na ‘show’ kamili. Kwa upande wa ‘highlight’ itaonyesha wa Mikoa, mafunzo mbalimbali ya muziki na safari nzima ya Bongo Star Search Msimu wa Kumi, hii itaruka kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa saa mbili na nusu usiku hadi saa tatu kamili usiku kupitia ST Swahili. Na kipindi cha wiki nzima ambacho kitakuwa na performance ya washiriki wote itaruka siku za Jumapili saa tatu kamili hadi saa nne Usiku kupitia ST Swahili pia.” Zamaradi
Chaneli ya ST Swahili ni chaneli namba 160 kwenye Antena na 400 kwa upande wa visimbuzi vya Dish. Pia chaneli hiyo inapatikana kuanzia kifurushi cha NYOTA kwa watumiaji wa Antena na Dish.


Habari njema zaidi kwa watanzania, tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI, TACAIDS imeingia ubia na StarTimes pamoja na BSS katika kufikisha ujumbe wake kwa watanzania.


“Kwa kutumia wasanii hawa watakaotumika tunaamini kuwa ujumbe wa namna ya kujikinga na maambukizi mapya ya VVU kupitia channel za Star times utawafikia watu wengi hasa vijana,ikiwa ni pamoja na kutangaza kuhamasisha umma kuchangia Mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI.” Jumanne Isango, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS.

(Visited 251 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us