ASSAs

NEDY MUSIC AFUNGUKA TOFAUTI YAKE NA JUX

1227
0
Share:

Nedy Music “Fine Boy” amepiga stori na EATV & EA Radio Digital, ambapo amefunguka kuhusu kuvimbiana na Jux, kununiana na Ruby pamoja na mengine mengi.

Akizungumzia kuvimbiana na Jux wakati wanarekodi wimbo wao mpya wa ‘Kinomanoma’ Nedy Music ameeleza,

“Hakukuwa na chochote kwa sababu hii ni kazi na sisi hatuko hivyo hata ukitutoa nje ya kazi ilikuwa fresh, tulikuwa tunashauriana vitu kama wasanii ili kuweza kutengeneza kitu kizuri na hatimaye tulikitengeneza hicho”.

‘Issue’ ya kununiana na Ruby baada ya kuchukua tuzo za ‘Afrimma 2018’ amesema, hakuna ugomvi wala kununiana kati yake na Ruby pia alijaribu kumtafuta kwa kila njia ili aonyeshe upendo na kumshukuru ila kama Ruby anasema hakumshuru atakuwa muongo.

Aidha Nedy Music amesema yeye hana maneno kama watu wanavyosema ila anazungumza kawaida na hachaguliwi cha kuzungumza na sio muongeaji sana huwa anaongea kawaida tu.

(Visited 111 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us