ASSAs

BEN POL AAHIDI KUACHA HISTORIA SIKU YA NDOA YAKE

333
0
Share:

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bernard Paul ‘Ben Pol’ ameweka wazi kuhusiana na maandalizi ya ndoa yake na mrembo wa Kenya Anerlisa kwa kusema kuwa siyo vizuri kujitapa kuhusu ndoa lakini anaamini yake itaacha simulizi kwa jinsi itakavyokuwa imepangiliwa.

Akizungumza na Amani, Ben Pol alisema kuwa kwa kimila kwa sababu tayari ameshatoa mahari ni kama ameshaoa bali bado tu kusimama mbele ya madhabahu kwa ajili ya kiapo.

“Ni kweli kabisa ndoa yangu inanukia na niko kimya kwa sababu sipendi kabisa kuinadi bali itakapofika kila mtu atamsimulia mwenzake kwa sababu itakuwa ya kistaarabu na isiyokuwa na mbwembwe nyingi lakini ya kipekee,” alisema Ben Pol

(Visited 37 times, 1 visits today)
Share this post