ASSAs

NANDY AELEZA SABABU YA KUMWAGA MACHOZI KABURINI KWA RUGE

513
0
Share:

Msanii wa Bongo flavour Faustina Charles Mfinanga amejikuta akishindwa kujizuia na kumwaga machozi kaburini kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba, unajua siri ya machozi hayo? Nandy ameitoa.


Akistorisha na Za Motomoto ya Risasi, Nandy aliyekuwa ameambatana na wasanii wenzake katika kaburi la Ruge kijijini kwao Kiziru, Bukoba mkoani Kagera, alisema machozi yake huwa yanashindwa kujizuia kila afikapo Bukoba.“Kila nikifika Bukoba lazima niende kuhani kaburi la Ruge. Nililia sana kwa sababu mbili; kwanza nakumbuka mengi aliyonifanyia, aliyonifundisha ikiwa kunifanya mpaka nimefika hapa nilipo na pili nilikuwa na wenzangu katika muendelezo wa Tamasha la Fiesta, hivyo kufika pale kumuenzi kwa umoja wetu niliumia sana kwani Ruge alikuwa mmoja wa waha masishaji,”alisema Nandy.

(Visited 29 times, 1 visits today)
Share this post