ASSAs

NANDY ALAMBA SHAVU DODO KUTOKA AZANIA

590
0
Share:

Mwanamuziki kutoka kiwanda cha Bongo flavour nchini Faustina Charles Mfinanga almaarufu kama Nandy amekula shavu baada ya kusaini mkataba na kampuni ya Azania Group of Companies kama barozi mpya wa kampuni hiyo.

Akizungumza wakati uzinduzi wa bidhaa ya Sabuni iliyotambulishwa na kampuni hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam Nandy ameeleza kuwa ni furaha kubwa kuona tasnia ya muziki inavyozidi kumsafirisha kutoka katika eneo moja kwenda eneo jingine.

“kwanza niwashukuru sana kwa kunipa fursa na kuniamini naamini ni kitu kikubwa sana kwangu, na labda niwahakikishie Watanzania hizi Sabuni ni nzuri na hawatajuta kuzitumia kwasababu hata mikono pia haichubui” amesema.

(Visited 48 times, 1 visits today)
Share this post