ASSAs

RAIS MAGUFULI ATOA AHADI KWA HAYATI BABA WA TAIFA

746
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuelekea miaka 20 ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, yeye ahadi yake ni kuendelea kuwaletea maendeleo Watanzania kama ilivyokuwa nia ya kiongozi huyo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Katavi, kwenye uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi katika barabara ya Mpanda, ambapo amesema kuelekea miaka 20 ya kifo cha muasisi huyo hana cha kuwaahidi zaidi ya maendeleo.

“Sisi tukiwa tunaelekea kuadhimisha miaka 20 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Nyerere nasema, sisi tuko pamoja na yeye katika kuwaletea maendeleo Watanzania”, amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli, ameagiza kubadilishwa kwa Halmashauri ya Mpanda na kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, kwa kile alichokieleza haiwezekani Wilaya iitwe Tanganyika, halafu Halmashauri iitwe Mpanda.

“Nimesikia Halmashauri hii inaitwa Mpanda District, wakati Wilaya ni Tanganyika sasa Waziri nenda ukabadilishe jina, iitwe Tanganyika District.” amesema Rais Magufuli

(Visited 61 times, 1 visits today)
Share this post