ASSAs

“HAKUNA KURA ZITAKAZO IBIWA WALA VURUGU ZITAKAZOTOKEA KIGAMBONI” DC SARA

440
0
Share:

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri amewatoa Hofu wakazi wa Kigamboni juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwataka wajitokeze kwa Wingi ili kuweza kujiandikisha.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam alipotembelea kituo cha kujiandikisha katika Daftari la wapiga kura katika kituo cha shule ya Msingi Vijibweni, amesema ndani ya wilaya hiyo hakutakuwa na ujanjaunja wala vurugu zitakazojitokeza.

“Iabda tu niwaambie wanavijibweni na wanakigamboni hakuna kura wala chochote kitakacho ibiwa, na ndio maana tunawahimiza mjitokeze mjiandikishe ili majina yatakapobandikwa basi mtaona na kujua maana mimi naamini mnajuana kwahiyo kama kuna mgeni basi mtaumbuana tu” amesema.

Katika hatua nyingine amefanya Zaira na kutembelea miradi iliyopo ndani ya wilaya hiyo ikiwemo kukagua Barabara, na madaraja yanayojengwa chini ya usimamizi wa TARURA, pamoja na kuwatembelea wananchi walio athirika na ujenzi huo.

Amesema zipo changamoto chache zilizosababisha mradi huo kusuasua ambapo amesema hadi kufika disemba 31,2019 anaamini atakabithiwa mradi huo ukiwa umekamilika.

Aidha amewataka wananchi wenye malalamiko yanayotokana na ujenzi huo ikiwemo wananchi ambao bado hawajalipwa fedha zao kutokana na kumegewa vipande vyao vya ardhi basi waweze kuandika barua na kuiwasilisha katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

“Kwanza tunamshukuru sana Rais wetu kwasababu anahitaji maendeleo katika wilaya yetu ya Kigamboni tayari tumeshapewa shilingi billioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara kutokea Kibada mpaka Pemba mnazi ambayo barabara hiyo ni ya kilomita 76 kwa hiyo changamoto za barabara katika wilaya hii tunazidi kuitatua kupitia Rais wetu” amesema.

Mradi wa Ujenzi wa barabara kutokea mjimwema mpaka Tungi imeghalimu kiasi cha shilingi 7.6 billioni ikiwa ni pamoja na kujenga Daraja ambapo mradi huo walikabithiwa TARURA Januari 1,2019 na unatakiwa kumalizika disemba 31,2019.

(Visited 27 times, 1 visits today)
Share this post