ASSAs

NAIBU WAZIRI WAITARA “Hakuna sheria ya Mwenyekiti kuomba hela ya Mhuri”

559
0
Share:

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara, amesema kuwa hakuna Sheria inayompa mamlaka Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, kuomba pesa ikitokea mtu au mwananchi anahitaji kujaziwa taarifa zake muhimu.

Waitara ametoa kauli hiyo leo Oktoba 28, 2019, wakati akizungumza katika kipindi cha East Afrika Breakfast cha East Afrika Radio,ambapo amesema ikitokea Mwenyekiti anataka kufanya hivyo, inabidi aitishe mkutano na wananchi ili waweke mapendekezo kulingana na mahitaji ya ofisi husika, kwakuwa wao huwa hawalipwi chochote na badala yake huwa wanategemea asilimia 20 ya posho inayotoka katika Manispaa.

Kwenye Serikali za Mitaa hakuna Sheria ya kutoa elfu tano au elfu 10, ukweli ni kwamba inabidi kiitishwe kikao na wananchi wajadiliane kutokana na mahitaji ya ofisi, mfano kununua samani za ofisi ama hela ya nauli ya kupelekea malalamiko mahakami au barua kwa Mkuu wa Wilaya, hivyo itabidi wakubaliane kwenye mkutano haitakiwi Mwenyekiti ajipangie kwamba kama mtu anataka kujaziwa fomu inabidi atoe elfu mbili au elfu tatu ila inabidi aitishe kikao na wananchi wakubaliane lakini wazingatie watu wasiokuwa na uwezo” amesema Waitara.

Akizungumzia suala la kuelekea katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Waitara amesema kuwa kuanzia Agosti 29 hadi Novemba 4, mtu anayepaswa kugombea nafasi hizo ni yule aliyepitishwa na chama chake kwa kuzingatia Sheia husika na kwamba Novemba 5 hadi 6, majina ya wagombea waliopitishwa kugombea yatabandikwa.

“Kuanzia kesho tarehe 29 hadi Novemba 4, tunataka mtu ambaye anapewa fomu ya kugombea awe amepitishwa na chama chake na tarehe 5 na 6 kutaanza kubandikwa kwa wagombea waliopitishwa kugombea.”

(Visited 121 times, 1 visits today)
Share this post