ASSAs

ZAHERA AWAJIBU YANGA ENDAPO ATAFUKUZWA

3261
0
Share:

Kocha wa klabu ya Yanga ,Mwinyi Zahera ameonekana kutokuwa na wasiwasi kuhusiana na mustakabali wake na klabu ya hiyo yenye makao makuu mitaa ya Jangwani na Twiga Dar es salaam.

Mara baada ya kupoteza mechi na Pyramids mashabiki waliokuwepo uwanjani waliaza kurusha chupa na kumtaka kocha huyo awaachie timu yao.

Shughuli ya kumtaka aondoke haikuishia uwanjani tu bali mashabiki hao waliendelea kurusha vijembe kwa kocha huyo kupitia mitandao ya kijamii na vituo mbalimbali vya televisheni na redio vilionekana kumponda mno.

 Mara baada ya kelele nyingi Zahera alitafutwa na akasema
” Sina wasiwasi endapo nitafukuzwa Yanga , kufukuzwa ni sehemu ya kazi kwani makocha wengi huajiriwa na kufukuzwa kwahiyo ni jambo la kawaida”

 kuna tetesi kuwa Kocha huyo ataondoka klabuni hapo mara baada ya mchezo na Pyramids kama watatolewa basi na yeye ataondoka.

Baadhi ya makocha wameanza kutafutwa na klabu hiyo yenye makao makuu mitaa ya Jangwani  na makocha hao ni Hans van der Pluijm.

Van pluijm mwenye uraia wa Uholanzi aliewahi kuifundisha Yanga kwa mafanikio makubwa kwa kuwawezesha kutwaa mataji mawili ya ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2014/15 na 2015/16 pia aliiwezesha klabu hiyo kucheza hatua ya makundi kombe la shirikisho.

Kocha mwingine aaewaniwa ni Mdenish Kim Poulsen aliewahi kuifundisha Taifa Stars kwa mafanikio makubwa.

Yanga wataondoka katikati ya wiki hii kuelekea nchini Misri wa ajili ya mchezo wa pili dhidi ya Pyramids utakaochezwa tarehe 03 Novemba katika dimba la 30 June Stadium uwanja wa nyumbani wa Pyramids 

(Visited 1,820 times, 1 visits today)
Share this post