ASSAs

MO DEWJI :YANGA RUKSA KUTUMIA UWANJA WA SIMBA-BUNJU KWA MAZOEZI

2130
0
Share:

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba Bw. Mohammed Dewji yupo nchini Uingereza kwa majukumu ya kibiashara. hapo jana alifanya interview na Salim Kikeke wa BBC Swahili 

moja ya Swali aliloulizwa kupitia mtandao wa Facebook  wa BBC Swahili lilisema : Je katika uwanja wa Bunju Yanga wataweza kuutumia kwa mazoezi?

Mohammed Dewji alianza kwa kusuasua kulijibu hilo swali na alianza kwa kusema:

“Itakuwa ngumu sana , kwanza wenzetu juzi walipata ajali na niliandika meseji na kuwaombea,unajua sisi tunataka ushindani na Yanga pia tunataka Yanga ipige hatua kama wengine. Unajua hakuna Simba bila Yanga na hakuna Yanga bila Simba .”

” La pili ni hakuna uhasama kati ya Simba na Yanga na tunaweza kutaniana na ndio maisha . Kama wao wakitaka kuja kufanya mazoezi na sisi kama hatufanyi mazoezi au tupo nchi nyingine au mikoa mingine tunaweza waruhusu hakuna shida “

Kwa kauli hiyo ya Mo Dewji klabu ya Yanga itaweza tumia uwanja wa bunju kwa mazoezi yao maana kauli ya mwekezaji huyo ni sheria na uongozi wa simba haupaswi kuikata . Tunafanya mipango wa kukutana na Voingozi wa Yanga kuona wameipokeaje kauli ya Mohammed Dewji.


(Visited 1,053 times, 1 visits today)
Share this post