ASSAs

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AZITAKA HALMASHAURI NA TAASISI ZA SERIKALI KUWA SOKO KUU LA BIDHAA NA HUDUMA ZITOLEWAZO NA VIKUNDI VYA VIJANA

469
0
Share:

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AZITAKA HALMASHAURI NA TAASISI ZA SERIKALI KUWA SOKO KUU LA BIDHAA NA HUDUMA ZITOLEWAZO NA VIKUNDI VYA VIJANANaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amezitaka Halmashauri za Manispaa,Wilaya na Majiji na taasisi mbalimbali za serikali nchini kuwa soko la bidhaa na huduma zinzatolewa na Vikundi na Kampuni za Vijana kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Vijana wazalishaji na watoa huduma ili kusaidia kuviimarisha na kukuza vipatao vyao.

Naibu Waziri Mavunde aliyasema hayo jana Jijini Tanga wakati wa ziara ya ukaguzi wa vikundi vya Vijana na watu wenye ulemavu vilivyowezeshwa kwa mikopo itokanayo na Mapato ya Ndani ya Halmashauri ambapo alitumia fursa hiyo kulipongeza Jiji la Tanga kuviwezesha vikundi hivyo na kuwataka waende mbele kuhakikisha wanawasaidia kupata pia masoko ya uhakika ya bidhaa zao ili vikundi hivi viendelee kukua zaidi na kuimarika.

“Naib Waziri wa Nchi Ofisi ya Kwenye kikundi hichi cha Ushonaji cha TAYOTAI mmekipa Tsh 100mza mkopo wa vyerehani,ni jambo jema na nawapongeza sana.Hakikisheni mnawasaidia pia kupata soko la nguo zao na ninyi Halmashauri ya Jiji muwe mfano kwa kushona hapa sare wa Watumishi wote wa Jiji ambazo mtazivaa kila Ijumaa na pia sare za shughuli zote za kiserikali ikiwemo wakati wa Mbio za Mwenge mchukue katika kiwanda hichi cha Vijana”Alisema Mavunde

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martin Shigella amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ndg Daud Mayeji kuhakikisha anasimamia utekelezaji wa maagizo ya Naibu Waziri Mavunde juu ya vikundi vya Vijana na wenye ulemavu vilivyopo Jijini Tanga vinavyozalisha bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kupewa kipaumbele katika shughuli mbalimbali za serikali ili kuvijengea uwezo wa kiuchumi.

(Visited 46 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us