ASSAs

OMMY DIMPOZ AJA KIVINGINE TUZO ZA AFRIMMA

1193
0
Share:

Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amemzidi ujanja msanii mwenzake, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ kwa kunyakua Tuzo ya AFRIMMA 2019. 

 Katika sherehe za tuzo hizo zilizofanyika hivi karibuni Dallas nchini Marekani, Dimpoz aliibuka kupitia kipengele cha Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki.

Katika komenti mbalimbali mtandaoni mara baada ya mkali huyo kunyakua tuzo na kufanya shoo kali, wengi walimgusia bosi wake, Ali Kiba anayemsimamia kupitia lebo ya Rockstar4000 kwamba amezidiwa.

“Wengi hatukutegemea kabisa kwanza kama tuzo hii itaenda kwa Dimpoz kutokana na ushindani uliokuwepo kwenye kipengele chake akiwemo Diamond na Kiba. Dimpoz ameonesha ujanja kwa hili na kuweza kumpiku hadi bosi wake,” alikomenti shabiki mmoja anayejiita Queen_aps.

“Kutoka kuumwa hadi kuwafunika Diamond na Kiba,” alikomenti shabiki mwingine Mzazi_Tulva. “Kuna cha kujifunza kwa Dimpoz kuchukua tuzo iliyokuwa ikionekana kwenda kwa Kiba au Diamond,” shabiki Suzy8 alikomenti.

Wasanii wengine waliokuwa wakishindania tuzo na Dimpoz ni Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Rajab Abdul ‘Harmonize’, Juma Musa ‘Jux’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ (wa Tanzania), Nyashinski, Khaligraph Jones (Kenya), Eddy Kenzo (Uganda) pamoja na The Ben wa Rwanda.

Wengine walioweka historia kwa kunyakua tuzo hizo ni Akothee wa Kenya aliyechukua kupitia Kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki akiwazidi ujanja Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na Faustina Mfinanga ‘Nandy’ wa Tanzania.

Pia Burna Boy wa Nigeria alichukua katika kipengele cha Msanii Bora wa Mwaka kwa Afrika akiwapiku Davido, Wizkid, Yemi Alade (Nigeria), Diamond (Tanzania), Busiswa na Black Cofee (Afrika Kusini).

Tuzo za AFRIMMA hutolewa kila mwaka tangu Disemba 27, 2014 na hafla hiyo iliasisiwa na Kamati ya Kimataifa AFRIMA, kwa ushirikiano na Umoja wa Afrika kutunza na kuzithamini kazi za wasanii, vipaji na ubunifu kote Afrika kwa nia ya kuhimiza utamaduni wa Afrika. Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo, Alikiba hajawahi kuambulia hata moja.

(Visited 144 times, 2 visits today)
Share this post

Contact Us