ASSAs

KINYOZI WA CRISTIANO RONALDO APIGWA HADI KUFA

3289
0
Share:

Kinyozi maarufu aliyekuwa anamyoa staa wa Jubentus na Ureno Cristiano Ronaldo amekutwa mefariki ndani ya chumba cha hotel nchini Uswizi.

Mwili wa kinyozi huyo umekutwa chumba cha hotel na mhudumu wa hoteli hiyo na alilipoti tukio hilo polisi. Kabla ya tukio hilo inasemekana uongozi wa hotel hiyo ulipokea simu nyingi kutoka kwa wateja wakilalamika kusikia kelele chumbani mwa Ricardo Marques. 

Mhudumu huyo anasema alipoingia chumbani mwa Ricardo alisikia harufu kali ya pombe na uuona mwili wa Ricardo. Polisi wanasema mara baada ya kufika mahali hapo walifanya upekuzi kila mahali lakini hawakuona silaha yoyote iliyotumika kumdhulu.

Inasemekana Ricardo mwenye asili ya Ureno amezaliwa na kukulia mji wa Madeira ambao Cristiano Ronaldo amezaliwa na kukulia hapo, Ricardo amekaa hotelini hapo kwa kipindi cha miaka miwili. 

Ricardo anasifika kufanya kazi na wanamitindo mbali mbali duniani na Ronaldo ni moja ya wateja wake wakubwa linapokuja suala la nywele.

(Visited 1,902 times, 1 visits today)
Share this post