ASSAs

ALICHOSEMA SAMATTA KABLA YA KUIFUNGA LIVERPOOL

2228
0
Share:

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Samatta hapo jana usiku aliweka rekodi mpya  ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuifunga Liverpool kwenye uwanja wake Anfield.

Samatta amekuwa mtanzania wa kwanza kucheza UEFA na kufunga bao dhidi ya Liverpool,pia amekuwa kapteni wa kwanza kutoka Tanzania kuiongoza Genk kwenye michuano hiyo.

Kabla ya mechi hiyo Samatta alifanya mahojiano na mtandao wa Ronaldo.com na alianza kwa kusema 

Nilipokuwa mdogo nilishabiki timu ya Manchester United, Kwa leo hatuongelei Manchester United bali Liverpool.
Tunafahamu Liverpool ni timu bora kuanzia ligi kuu Uingereza na hata michuano ya ulaya , tunafahamu itakuwa gemu ngumu ila  tutajitahidi kuwafunga  
Kila mtu nyumbani ( Tanzania) anazungumzia mechi hiyo na wanatamani kuniona nikimpiga chenga beki bora wa dunia Van Vigri Dijk na nafikili watu wengi watakuwa wnaangali mchezo huu”
Mchezo wa Liverpool na Genk ulimalizika kwa Genk kufungwa mabao 2-1 huku bao pekee la Genk likiwekwa kimiani na Samatta .

(Visited 1,327 times, 1 visits today)
Share this post