ASSAs

KESI YA ALIYEMCHOMA MKE WAKE KWA MAGUNIA YA MOTO YAFIKIA HAPA

1321
0
Share:

Leo Jumatatu, Novemba 18, 2019, katika Mahakama ya Halimu Mkazi Kisutu kesi inayomkabili mfanyabiashara Hamis Luwongo (38) anayedaiwa kumuua kisha kumchoma moto mkewe, Naomi Marijani kwakutumia magunia mawili ya mkaa, upande wa jamhuri umeeleza kuwa jarada la kesi hiyo lipo katika hatu za mwisho la uchapaji.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon Mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Salum Ally amesema kuwa jarada lipo kwenye hatua ya mwisho ya uchapaji na baada ya hapo linatakiwa lipelekwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria.

Kwa upande wake Wakili wa utetezi, Mohammed Majaliwa alisema hana pingamizi na ombi hilo, hivyo hakimu Salum Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 2 mwaka huu na mshtakiwa amerudishwa rumande.

Mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.

(Visited 288 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us