ASSAs

FAHAMU NJIA ZA KUONDOA MADOA USONI

679
0
Share:

Watu wengi huwa wanateseka usoni kutokana na madoa yanayobaki kutokana na chunusi na hii inatokana na kitendo cha kuzitumbua chunusi zikiwa hazijaiva, basi leo nimekuwekea baadhi ya njia ambazo ukizitumia utaweza kuondoa madoa usoni.

1: Juisi ya limao na liwa
Chukua juisi ya limao kiasi changanya na liwa kisha paka eneo lililoathirika, kaa kwa muda wa dakika tano utaona matokeo.

Image result for juice ya limao

2: Juisi ya limao na unga wa mdalasini pia ni tiba nzuri ya kusafisha uso kuondokana na madoa yote na chunusi zote.

Image result for juice na mdalasini

3: Asali na mdalasini
Chukua vijiko vitatu vya asali na kimoja cha mdalasini changanya kisha paka usoni pia ni tiba nzuri inasaidia kwa kiasi kikubwa.

Image result for mdalasini

4: Apple na asali
Chukua apple liponde changanya na asali kiasi, kisha paka usoni mbali na kutibu madoa pia inatibu chunusi.

Image result for apple na asali

5: Maji ya kitunguu swaumu

chukua maji ya kitunguu swaumu paka kwenye madoa yote utaona matokeo.ponda ponda kitunguu swaumu kisha loweka kwa muda wa nusu saa tumia yale maji

Image result for maji ya kitunguu swaumu

6: Nyanya
chukua kipande cha nyanya paka usoni kisha kaa kwa muda wa saa moja nayo ni tiba nzuri.

Image result for nyanya

7: Tango

Tango pia ni tiba, chukua kipande sugua uso wako kila siku asubuhi utaona matokeo.

Image result for tango tunda

8: Papai
Chukua papai liponde kisha paka usoni litakusaidia kuondoa tatizo la madoa yote usoni.

Image result for papai tunda
(Visited 80 times, 1 visits today)
Share this post