ASSAs

FAHAMU NJIA ZA KUMFANYA RAFIKI YAKO KUWA MPENZI WAKO

6789
0
Share:

Kumpenda mtu ni kitu kingine lakini kumfanya awe na hisia kama zako juu yako ni kitu ambacho kinahitaji zaidi ya mahesabu na polojo za kumshawishi mtu huyo.

Ukiacha bahati ya kuvutiana ghafla (love in first place), uhusiano wa kimapenzi unazingatia ‘theories’ za kisayansi za uhusiano na jinsi ya kuuteka ubongo na hatimaye moyo wa mtu unayetaka kuwa naye, hususan ambaye mnaweza kuwasiliana kama marafiki.

  1. Tumia Mitandao ya Kijamii, Charting

Katika karne hii karibu warembo wote wako katika mitandao ya kijamii. Kama hawako Facebook, Ello na mingine basi simu zao za kiganjani huwa na app ya Whatsap. Fahamu rafiki yako huyo unayetaka kuwa naye anapendelea mtandao gani kati ya hiyo, ukifanikisha anza kuwasiliana naye. Mtumie jumbe zinazozaa jumbe kadhaa na kuvuta usikivu wa kuwasiliana. Anza kidogo kidogo kwa kumfahamu. Usiwe na haraka ya kutaka majibu. Endelea kuwasiliana naye taratibu lakini kila unachowasiliana naye hakikisha unakiwaza na kukipanga vizuri. Kupitia jumbe zako anaweza kuanza kuvutiwa kuwasiliana na wewe kama rafiki, na hapo unaweza kuendelea kudumisha mawasiliano na kuonesha ‘busara’, kujali na mengine kama anavyoonesha kusogea. Usikurupuke.

Kwanini mitandao ya kijamii na sio jumbe za kawaida kwenye simu? Tafiti zinaonesha kuwa mitandao ya kijamii humvutia mtu kutuma jumbe na kufurahia mjadala zaidi ya jumbe za kawaida (SMS).

          2. Mwambie Mambo yote Kuhusu Wewe lakini sio ‘kila kitu’

Wengi hupenda kuwafahamu kiundani watu ambao wako nao karibu hasa katika uhusiano wenye muelekeo wa kimapenzi. Weka vitu vyako mezani. Lakini chagua kwa makini, mwambi ahisi umemwambia yote aliyotaka kufahamu kuhusu wewe, lakini usimwambie kila kitu kwa kuwa uwazi uliopitiliza utakukosesha ‘points nyingi’. Tunza maneno yako atamani kusikia zaidi kutoka kwako.

     3. Onesha Hisia Zako Kifikra zaidi ya Kivitendo

Mfanye ugundue hisia zako kwa kukutazama na kusikiliza maelezo ya kawaida unayoongea naye. Jinsi unavyomjali na mengine. ‘Mental Emotions’ zinashika zaidi na zina nguvu kuliko ‘physical emotions’. Mfanye atumie dakika zake kadhaa kukufikiria hata kabla hujamwambia ‘Nakupenda’. Kifikra utakuwa umeshasema mengi kwake na atabaki kuwa mchambuzi na ataanza kuvutika kwako.

     4. Adimika

Siku zote kitu adimu huengezeka thamani zaidi. Jitahidi kuwa adimu kwake wakati mwingine ili umpe nafasi ya kukumiss. Hisia zako zinaongea kwa sauti kubwa zaidi kwake. Ukiwa unapatikana kila wakati kwa ajili yake atafikia hatua hatakuwa na muda mzuri wa kuvuta fikra kukukumbuka. Adimika ila usipotee.

(Visited 4,662 times, 1 visits today)
Share this post