ASSAs

FAHAMU MAISHA NA SIFA ZA TEMBO

661
0
Share:

Tembo ndio mnyama pekee ambaye ni mkumbwa kuliko wote anayepatikana ardhini na inaelezwa kwamba tembo dume mkubwa  huweza fikia takribani kilo 2000 – 6000 (Tan 2- Tan 6) huku jike akiwa na kilo 2000-4000 (Tan2-Tan4).Mbali na hayo mtoto wa tembo huzaliwa akiwa na kilo zisizo pungua 120.

Kuna mengi ambayo humuhusu mnyama huyu na ambayo huwezi kuyakuta kwa mnyama mwingine wa porini miongoni mwa hayo mengi ni pamoja na haya yafuatayo…

 •       Tembo wanahuwezo wakusikilizana umbali wa kilomita 8.
 •      Tembo wa Afrika wanahisia nzuri kuliko mnyama yoyote.
 •   Tembo huogopa nyuki.
 • ·   Ukiacha na binadamu, tembo ndio mnyama mwenye kidevu.
 • ·   Tembo ni mnyama ambaye hulala mda usio pungua masaa mawili hadi matatu kwa siku.
 •    Tembo huhitaji takribani kilo 300 kwa siku na lita 160 ili kumuwezesha kushiba, na chakula chake ni majani, magome ya miti, mizizi pamoja na matunda.
 •   Tembo ndio mnyama pekee anayebeba mtoto tumboni (mimba) kwa kipindi cha muda mrefu kuzidi wote dunia ni miezi 22, na mtoto hutoka mmoja tu.
 • ·  Tembo hushika mimba kila baada ya miaka miwili
 •     Meno ya tembo hukaliliwa kufika kilo 200 (yote mawili)
 • ·   Kundi la tembo au Familia ya tembo huongozwa na jike
 •     Tembo ni mnyama mwenye kumbukumbu nzuri
 •    Tembo akiwa porini huweza kuishi takribani miaka 60-65.
 •  Tembo anaanza kutokwa na meno ya nje baada ya miezi kumi na sita ila ifikapo miezi 30 ndio huuanza kuonekana.
 •   Kinyesi cha tembo huaminika kuwa ni dawa.
 • Tembo ni miongoni mwa wanyama anayepatikana katika hifadhi zetu hapa nchini yapaswa kujivunia na kuwatunza kwa faida ya vizazi vijavyo pia

(Visited 73 times, 1 visits today)
Share this post