ASSAs

ELIMU YA UFUNDI NA TEHAMA KUBORESHWA TANZANIA

567
0
Share:

Na Mwandishi Wetu

WADAU mbalimbali wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wamekutana katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) kujadili namna ya kuboresha elimu hiyo.

Wakijadili mradi wa Kituo cha Umahiri wa Tehama (RAFIC) uliopo DIT, Mratibu wa Mradi huo unaofadhikiwa na Benki ya Dunia, Joseph Matiko anasema mradi huo utasaidia kuboresha elimu ya ufundi pamoja na TEHAMA ili kuweza kuzalisha vijana watakaotumika katika kusaidia mapinduzi ya viwanda.

“Wadau wa TEHAMA muhimu kujadiliana kuona namna gani mtatusaidia katika hatua mbalimbali za utengenezaji wa mitaala na namna gani tutavyowashirikisha kwenye shughuli za uendeshaji,” anasema Matiko.

Katika mradi huo tutajenga jengo la kisasa, ununuzi wa vifaa vya kufundishia maabara vya kisasa, ofisi ya za walimu, maktaba na mabweni ya wanafunzi kutoka nje ya nchi na nyumba za kuishi wakufunzi wageni.

(Visited 62 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us