ASSAs

HAWA HAPA WAFUNGWA WALIOACHIWA HURU SIMIYU

1122
0
Share:

Kufuatia msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alioutoka Desemba, 2019 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika jijini Mwanza wafungwa 136 kutoka magereza za Mkoa wa Simiyu wamechiwa huru

Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Disemba 10, 2019 Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP. Andulile Mwasampeta amesema anamshukuru Mhe. Rais Magufuli kitendo hicho cha kutoa msamaha ambacho kimesaidia kupunguza msongamano kwenye magereza ya mkoa wa Simiyu.

“Ninamshukuru sana Mhe. Rais Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwa kutoa msamaha huu ambao umepunguza msongamano katika magereza yetu hususani gereza la Bariadi; nitumie nafasi kuwaasa wafungwa waliosamehewa kwenda kuwa raia wema na wakafanye kazi halali na wasifanye makosa yatakayowaleta tena hapa gerezani,” alisema ACP Mwasampeta.

ACP Mwasampeta ameongeza kuwa wafungwa 136 waliopata msamaha wa Rais katika mkoa wa Simiyu ni wale waliokuwa wamebakisha muda wa siku moja hadi miezi sita miezi 12 kumaliza muda wa vifungo vyao, ambapo amebainisha kuwa wamezingatia maelekezo ya Mhe. Rais katika vigezo vya watu walioachiwa huru.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa kufanikisha zoezi la kuwaleta pamoja wafungwa wote waliopata msamaha wa Rais kwa kutoa magari yaliyowezesha jeshi la magereza kuwachukua katika magereza mbalimbali mkoani Simiyu na kuwaleta katika gereza la Bariadi ambapo ndipo walipoanzia safari ya kurejea majumbani kwao.

Kwa upande wao wafungwa waliopata msamaha wa Rais na kuachiwa huru wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutoa msamaha huo na kuahidi kuwa raia wema watakaofanya kazi halali na kujiepusha na makosa yote yanayoweza kusababisha wakarudi tena gerezani.

(Visited 130 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us