ASSAs

INFINIX S5 O- Display, KAMA NI UPANA, BASI NI PANA HASWAAA!

565
0
Share:

Matoleo mapya kutoka Infinix, yani Infinix S5 na Infinix S5 Lite yametua mjini. Sasa wadau wanasema kwa Kioo cha O-Display, kama ni upana basi pana haswaa lakini sio hilo tu, kuna mengi tumejionea kutoka simu janja hii. Kama ulikua hujui, basi hizi ndio sifa zinazoifanya Infinix S5 iibuke kidedea.


Ukiachilia mbali kamera ya mbele kuwa na uwezo mkubwa wa 32 MP, teknolojia ya AI iliyopo kwenye kamera hii inasaidia kuhifadhi picha zako kwenye “cloud” hata kama nafasi kwenye simu yako ikiwa imejaa. Upo hapo? Na bado, wadau mbali mbali wametumia kamera ya Infinix S5 kwenye mazingira tofauti tofauti ikiwemo mazingira yenye mwanga hafifu na picha ni ang’avu tayari kwa kushare mitandaoni!

Kama ulidhani tumemaliza kwa upande wa kamera basi umekosea. Simu janja hii inakuja na kamera 4 za nyuma kuzipa picha zako mtazamo nadhifu kwa mazingira ya aina yoyote

Sikia sasa mdau, Infinix S5 ina mng’ao flani hivi wa kukupa heshima mjini. Umbo lake linakifanya kifaa hichi kutulia mkononi bila wasiwasi wa kudondoka. Muonekano huu wa Infinix S5 ni wa kipekee ni sababu tosha ya kujidai unapokuwa na marafiki.

Na hapo bado hatujamaliza, cha kitofauti tulichogundua, ukiwa na Infinix S5 unweza kuiseti simu yako kama utakavyo. Chagua mifumo unayoitaka wewe na uifanye simu yako iwe nyepeeesi kama unyoya. Huna haja ya kudownload apps zisizo salama, simu ya Infinix S5 ina ulinzi Madhubuti. Yani ni wewe tu na uhuru wa utakacho katika simu yako.

MTK P22, 4/6 GB RAM, 4000mAh tuendeleee? Vyote hivi vinaipa Infinix S5 uwezo wa juu wa kufanya kazi, yani chombo kimesimama. Hofu ya kuishiwa betri hakuna na unweza kutumia apps nyingi kwa wakati mmoja bila kwikwi!

(Visited 226 times, 1 visits today)
Share this post