ASSAs

NJIA ZA KUMFANYA MPEZI WAKO AKUWAZE MUDA WOTE

8743
0
Share:

Kuweza kumpata na kumteka mwanaume akili zake siyo kazi rahisi. Haya hapa   mambo ambayo yatamfanya mwanaume aachane namambo yake yasiyoeleweka na abaki akikuangalia na kukutafakari hadi aseme Daah kweli huyu ni mwanamke wa kipekee.

Jiamini.

Najua hii umeshazoea kuisikia pia. Kujiamini kunavutia. Inamaanisha unajitambua wewe ni nani na unataka dunia nzima ijue wewe ni nani – na wanaume hupenda hili. Achana na madhaifu yako yote na jiamini ulivyo lazima atakupenda tu.

Jiheshimu.

Hakuna kitu kisichovutia kwa wanaume kama mwanamke asiye jiheshimu. Wanaume hujua- kama unaweza ukaonesha tabia za kutokujiheshimu mwenyewe – unawezaje kumshawishi kwamba unaweza kuwaheshimu wengine? Kwa wewe kujiheshimu kutamfanya macho yake na mawazo yake yakuwaze wewe tu!

Kuwa Mpole, Mtulivu, Mwema.

Unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza – anachokiona ndivyo atakavyokutafsiri. Kuwa mkarimu na mpole ni kitu kikubwa sana mwanaume atakachovutiwa nacho kwako. Kama wewe ni mkarimu kwake na kwa watu wanaomzunguka, ata assume kwamba wewe ni mkarim kwa ujumla, na wanaume sikuzote hutafuta lulu ya hivi kwa mwanamke.

Kuwa muelekezi.

Usifanye hayo makosa. Wakati baadhi ya wanaume wanaweza kuipenda hiyo tabia(wachache sana), ila hubadilisha mambo baada ya mjda fulani. Kuwa unatoa amri ni moja wapo ya njia zitakazomuonesha unaweza kuwa kiongozi / msimamizi wa kitu fulani. Maranyingi , wanaume wengu hudhani kuwa wao ndoyo mara nyingi wanatakiwa kuwa viongozi kwa kila jambo, na ni kweli huwa ni vizuri anapoagiza jambo na mwanamke analitekeleza lakini na wewe uoneshe unaweza kusimamia unachoelekezwa nae!

Jijali wewe na mambo yako.

Simaanishi uwe unaishi kama miss Africa – Hapana! Ninachosema unatakiwa uyaweke mambo yako katika muundo na mpangilio unaoeleweka ambao ni rafiki kwako na mambo yako. Fanya mazoezi, kula vizuri, na kuwa msafi ni tabia ambazo wanaume wengi huvutiwa nazo. Kwanini? Kwa sababu inamaanisha hautaki tu ufanye kazi zako lakini ufanye uku hali yako ya afya ikiwa inaimarika, lakini pia uwe wa kupendeza na kunukia vizuri karibu yake.
Kama ataona unajijali, atajua ua uwezo mkubwa wa kujiwajibisha – kitu ambacho hukipenda sana

Usiwe wa kusomeka haraka.

Usijaribu saana kumfanya yeye akupende. Kuwa makini sana na matendo yako wakati upo mbele yake – asikusome lengo lako hasa ni nini. Mfanye awe na maswali juu yako ya kuwa wewe ni wa aina gani. Hii itampa picha ya kwamba unajijali wewe na mambo yako lakini pia unatambua uwepo wake.

Kuwa muwazi.

Ni ngumu sana kwa mwanaume kukupenda na kumteka mawazo yake kama hakujui vizuri!. Funguka kwake. Sasa usianze kuropoka mambo yote yanayokuhusu kwake – utaharibu. Hatajali eti kwamba wewe kuna jamaa alikukatili wiki moja iliyopita na akakufanya ulie siku nzima.

Mwambie matazamio yako, malengo yako na ndoto zako. Mpe mawazo na mitazamo yako kwa baadhi ya mambo yanayoendelea katika jamii inayowazunguka au hata katika nchi. Kwa kumfanya akujue wewe ni wa aina gani , na ndoto zako na malengo yako, itamfanya akuone wewe wa tofauti na shujaa! Niamini

(Visited 6,004 times, 1 visits today)
Share this post