ASSAs

WAKALA WA MISITU YAZINDUA KAMPENI YA KI-NATURE KWA KISHINDO

320
0
Share:

Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kampeni maalum ya kutangaza utalii nchini lengo likiwa ni kukuza uchumi wa nchi pia.

hayo yamesemwa na Meneja Masoko na uwekezaji Wakala wa Misitu Tanzania Mariam Kobelo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leoi jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampeni maalum ya twenzetu ki-Nature inayotarajia kufanyika tarehe 17 Disemba hadi 20 disemba mwaka 2019.

Kobelo amesema kuwa kampeni hiyo ipo chini ya Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangala, ambapo amebainisha maeneo hayo kuwa ni pamoja na Bagamoyo Pwani, ziwa Ngosi Kalambo, Amani Tanga, Msitu Pugu, Same Meru na maeneo mengine ambayo kwa idadi yake ni maeneo 17.

“Serikali iliona kuna uzuri wa kipekee katika hiyo misitu ipo 17, mbali na wanyama lakini pia kuna vivutio vingi natoa wito kwa watanzania kuweza kujitoakeza kwa wingi kutembelea hii pia ni faida kwa nchi kwasababu itasaidia kukuza Pato la Taifa

Na kwa kuanza kampeni hii Tutaanzia Pwani Bagamoyo Serikali inajitahidi kuweka watu pamoja ili kusaidia utalii kuzidi kukua, hivyo tunawaomba Watanzania kufika katika Ofisi za wakala wa Misitu ili waweze kujifunza vitu vingi” amesema.

ameongeza kuwa “Ki- nature ni utalii unaohusiana zaidi na misitu hivyo tukienda hatufikilii kukutana zaidi na wanyama tuliowazoe Bali vitu vidogo vidogo lakini vya kipekee vya kuvutia yaani.”

Aidha uzinduzi huo ulijumuisha wadau mbalimbali akiwemo Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth Makunde ambaye pia ni Balozi wa Utalii amesema anaamini kupitia kampeni hiyo itasaidia watanzania kuweza kufahamu umuhimu wa Utalii ndani ya Taifa.

“Nilipokuwa miss Tanzania nilipata fursa ya kujifunza vingi vya utalii, me niwaombe Watanzania katika msimu huu wa sikukuu basi tujitokeze kutembelea hizi hifadhi na tuweze kujifunza vitu vingi sana” amesema Elizabeth.

Naye muigizaji na Muandaaji wa filamu nchini Jacob Steven almaarufu kama JB kupitia ziara hiyo anaahidi kuwa balozi mzuri wa kutangaza utalii na vivutio mbalimbali kupitia katika filamu ambazo anategemea kuzifanya na kutumia maeneo hayo kama moja ya sehemu ya filamu hizo.

“Kipekee naishukuru sana Wizara naamini hii ni fursa kubwa sana kwangu maana nimeweka historia ya mtu mwenye uzito mkubwa duniani kupanda mlima huo, na imewamotivate watu wengi.

Kama muuandaji wa filamu hii ni fursa kubwa kwasababu tunapoaandaa filamu pia tunahitaji kuangalia mazingira hivyo nawashukuru sana TFS maana pia tutaitangaza nchi kwasababu sisi tuna kazi kubwa ya kutangaza nchi” amesema JB

(Visited 35 times, 1 visits today)
Share this post