ASSAs

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATOA AGIZO KUTOLEWA KWA MAKAMANDA WAWILI

260
0
Share:

Kutokana na Makamanda wa Polisi wa Mikoa Miwili ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba kushindwa kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 16 za Makazi ya Polisi uliozinduliwa mwishoni mwa mwaka 2018 na Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemuelekeza Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini, Simon Sirro kuwaondoa.
Masauni ametoa agizo hilo jana Alhamisi Desemba 12, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Unguja.

Amesema kwa muda mrefu kisiwa cha Pemba kimekuwa na matukio yasioridhisha jambo linaloashiria kuwa wameshindwa kazi.

Makamanda hao ni Hassan Nassir Ally wa Mkoa wa Kusini Pemba na  Sheikhan Mohamed Sheikhan wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akitoa mfano wa matukio hayo, Masauni amesema Maalim Seif anafanya mikutano kila kona huku ikijulikana kuwa imezuiwa.

(Visited 29 times, 1 visits today)
Share this post