ASSAs

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO DISEMBA 15, 2019

381
0
Share:

Barcelona inasubiri pembeni kumuajiri kocha wao wa zamani Pep Guardiola iwapo ataamua kuiaga miamba ya ligi ya Premia Manchester City mwisho wa msimu huu.. (Sunday Express)

Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi Guardiola iwapo raia huyo wa Uhispania atandoka katika klabu hiyo ya Uingereza(Sun on Sunday)

Pep Guardiola

Mshambuliaji wa klabu ya Red Bull Salzburg, mwenye umri wa miaka 19 na raia wa Norway Erling Haaland ameweka wazi kwamba Man United ndio klabu anayolenga kuhamia iwapo ataondoka katika klabu yake mwezi Januari.. (Star on Sunday)

Unai Emery
Image captionAliyekuwa mkufunzi wa Arsenal Unai Emery kabla ya kufutwa kazi na klabu hiyo

Makocha wanaopigiwa upatu kumrithi Unai Emery katika uwanja wa Emirates wanazuiwa na hali ya klabu hiyo kutotaka kununua wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho.. (Express)

Manchester City imeajiandaa kushindana na Manchester United, Liverpool na Chelsea katika kumsajili upya winga wa Uingereza mwenye kwa thamani ya £90m Jadon Sancho, 19. (Sun on Sunday)

Mkufunzi wa West Ham Manuel Pellegrini anakaribia kupigwa kalamu licha ya timu yake kupata ushindi siku ya Jumamaosi huku kocha wa zamani David Moyes akitarajiwa kujaza pengo lake. (Star on Sunday)

Jadon Sancho
Image captionMchezaji wa Borussia Dortmund anayepigiwa upatu kujiunga na Man United Jadon Sancho

Chelsea imeweka dau la 30m euros (£25m) kwa klabu yoyote inayotaka kumnunua beki wa kushoto wa Uhispania Marcos Alonso, 28. (Calciomercato)

Manchester United inafikiria kumnunua mshambuliaji wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens, 32. (Tuttomercato)

Klabu hiyo ya Old Trafford pia inafikiria uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan raia wa Argentina Lautaro Martinez, 22, na kiungo wa kati wa Paris St-Germain Leandro Paredes, 25. (Mirror)

Marcos Alonso
Image captionBeki wa kushoto wa Chelsea na Uhispani Marcos Alonso

Kiungo wa kati wa Chelsea N’Golo Kante, 28, anataka kuondoka katika klabu hiyo lakini atapuuzilia mbali ushauri wa mchezaji mwenza wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kuelekea Juventus au Real Madrid badala ya Barcelona. (Eldesmarque)

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Eden Hazard, 28, ameapa kurudi klabu yake ya zamani mkataba wake Real Madrid utakapokamilika . (Sun on Sunday)

Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho anasema kwamba hatofichua maelezo ya mazungumzo yake na kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen kuhusu hatma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Sunday Mirror)

Eden Hazard
Image captionMchezaji wa zamani wa Chelsea Eden Hazard anasema yuko tayari kurudi katika klabu yake ya zamani atakapomaliza mktaba wake Real Madrid
(Visited 48 times, 1 visits today)
Share this post