ASSAs

LIVERPOOL KUMSAINI STRIKER WA RB SALZBURG

1541
0
Share:

Liverpool muda wowote ule itatangaza kumsaini striker wa RB Salzburg, Takumi Minamino ambaye leo hii inaamina kuwa atakuwa kwenye vipimo vya afya.

Minamino impressed against Liverpool in both games in the Champions League group stage

Minamino akiwa katikati ya msitu wa Liverpool kwenye mchezo wa Champions League hatua ya makundi

Mjapani huyo mwenye umri wa miaka 24, inadaiwa ameingia kandarasi  ya miaka minne na nusu ya kuwatumikia klabu hiyo yenye maskani yake Anfield huku dau lake likidaiwa kuwagharimu hte Reds pauni milioni 7.25 ikiwa na kifungu cha kumuachilia nyota huyo.

Mpaka sasa majadilian kwa pande zote mbili baina ya Liver dhidi ya klabu hiyo yenye maskani yake Austrian yamekwenda vizuri na kilichobakia ni utaratibu tu.

The Japan international is a versatile player and can offer cover for Liverpool's front three

Jurgen Klopp hataki kupotaza muda kabisa anatarajia kumjumuisha Minamino mara tu baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili Januari 1.

Nyota huyo wa Japan anatarajiwa kuanza majukumu yake kwa waajiri wake hao wapya kwenye mchezo wa FA Cup, Merseyside derby dhidi ya Everton kama ilivyokuwa kwa beki bora kwa sasa duniani Virgil van Dijk alivyowahi kufanyiwa miaka miwili iliyopita.

Kwa namna ratiba ilivyo wabana majogoo hawa wa England ambao kwa sasa wapo Qatar kwaajili ya Club World Cup, kumuongeza kijana huyo Minamino kutawasaidia wengine kupata muda.

Minamino anauwezo wa kucheza mbele ya wachezaji watatu ama namba 10, ingawaje atakuwa na kibarua kizito kutokana na nafasi hizo kuwa na nyota hatari Roberto Firmino, Mo Salah na Sadio Mane ambao kila mmoja yupo fiti.

Minamino mpaka sasa ana jumla ya mabao saba na ‘assists’ tano katika michuano yote aliyocheza msimu huu.

(Visited 257 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us